November 29, 2020

 



IKIWA leo Novemba 29 Simba wanashuka Uwanja wa New Jos kusaka ushindi mbele ya wapinzani wao Plateau Unted kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika mambo yamezidi kuwa magumu kwa wapinzani hao kuendelea kufanya mipango ya kuwatoa mchezoni Simba.

Kazi kubwa leo itakuwa kwenye kusaka ushindi ndani ya uwanja na ikiwa wawakilishi wa Tanzania Simba hawatakuwa makini basi wanaweza kupoteza mchezo wa leo kutokana na mambo ambayo wamekutana nayo.

Awali baada ya kufika  mji wa Jos ambapo ndipo ipo kambi ya wapinzani wao Plateau United ilielezwa kuwa wachezaji na viongozi wa Simba waligomewa kutumia wapishi wao maalumu jambo lililoanza kuwavuruga mwanzo.

Pia kabla ya mchezo kuchezwa inaelezwa kuwa kulikuwa na mpango wa kuwatoa wachezaji muhimu kikosini ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Luis Miquisssone, John Bocco na Jonas Mkude kwa kutaka waonekane na Virusi vya Corona ili wasicheze mchezo wa leo.

Pia wapinzani hao ambao waliwahi kuingia kwenye kashfa ya kupanga matokeo ndani ya Nigeria wamegomea mchezo kuonyeshwa mubashara.

Kupitia kwa Mtendaji Mkuu wa Simba, (CEO) Barbara Gonzalez amesema:- “Plateau United wamekataa kuruhusu mechi kurushwa mubashara. Licha ya juhudi zetu zote tukishirikiana na mshiriki wetu AZAM TV, mwenyeji wetu amekataa kushirikiana kwenye hilo.

"Nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa wapenzi wetu wote ulimwenguni ambao walitaka kuangalia mechi hii. Mpaka muda huu, tunapigania hii mechi iweze kuoneshwa mubashara (live).” 



12 COMMENTS:

  1. Mbona kelele nyingi? Nyinyi jipangeni kwa ajili ya mechi uwanjani; si mna kikosi kipana? Kelele za nini oooh figisu, oooh hujuma, ooh zengwe be serious and focused, mpira hauchezwi kwa propaganda

    ReplyDelete
    Replies
    1. We upotolo mechi za kimataifa hazikuhusu endelea kucheza mchangani

      Delete
    2. Hayakuhusu endelea kusugua benchi kimataifa wacha wanaume wafanye Yao. Ww ushambwela kimataifa endelea kusugua benchi na utopolo wako na utopolo wenzio. Wanaume wanaojielewa wanafanya Yao kitaifa na kimataifa
      Funga Domo 🤫 iwazie ihefu bdo level yako.

      Delete
  2. Kikubwa km wawakilishi wa taifa, yatakuwa Kupambana bila kujali changamoto zilizopo, wao si wanaanza kwao? Basi nanyi mje kumaliza kwenu, pambaneni kikubwa msiruhusu goli zaidi ya moja km draw itashindikana, nawaamini na watanzania tunawaamini, naweka pembeni uyanga wangu, niwatakie kila la kheri, watani

    ReplyDelete
  3. Na bado Boko haramu hawajaja kuwateka wachezaji wote munaosema ni muhimu, yani watawapangia hadi kikosi Leo nguruwe fc nyie, mnaanza kuwadanganya mikia fc wenzenu et mnaletewa figisu mara et zengwe, nyie kipindi Al Ahl na As vita zinawapiga Khasa mbona hamkusema kuwa kuna zengwe? Cheza mpira si mnakikosi kipana ? Au mwende polisi au TTF kama mlivyozoea

    ReplyDelete
  4. Da!co ratiba kamili kuhusu kuonyesha kwa mchezo wa simba vs plateau aitoonyeshwa

    ReplyDelete
  5. Nigeria Kama Ni kweli wanachofanya Ni mambo ya kizamani na aibu tupu kwa taifa hilo kubwa kisoka, kinachionekana na mchecheto baada ya kubaini wanakutana na mziki mnene wa SSC. Ila kwa kutokuruhusu mechi kurushwa live siyo fair hata kidogo. Kinachonisha gaza utadhani hawajui figisu wanazofanya nao wanaweza wakafanyiwa figisu hizo hizo wakitua hapa Tz.

    ReplyDelete
  6. Waache wafanye figisu zao zote ila wajuwe tu goli 3 zinawasubiri inshaallah imekula kwao wakija dar wanapigwa mkono ww subiri tu wataona cha moto

    ReplyDelete
  7. Wachezaji wawe makini Sana na faulo, wanapaswa wacheze kwa tahadhari kubwa kwa kuwa Kuna uwezekano mkubwa wa kupewa kadi mfululizo ili kupunguzwa kasi, kwa kuwa mechi hii uwezekano mkubwa itachezeshwa na waamuzi wa ukanda wa West Africa. Hii bench la ufundi wa take note.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic