KOCHA Mkuu wa Wolves, Nuno Espirito Santo amesema kuwa ana furaha kubwa kumuona nyota wake wa zamani Diogo Jota akifanya vizuri ndani ya kikosi cha Liverpool chini ya Kocha Mkuu Jurgen Klopp.
Wolves ilimuuza mshambuliaji huyo kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kwa dau la pauni milioni 14 kwenye usajili wa Septemba.
Tangu atue ndani ya Anfield, Jota ameweza kufunga jumla ya mabao saba na mabao yake sita amefunga kwenye mechi nne za mwisho ambazo alipewa nafasi ya kucheza na alipiga hat trick yake ya kwanza dhidi ya Atalanta kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Nuno amesisitiza kwamba hakuna ubaya kwa nyota huyo mwenye miaka 23 kufanya vizuri akiwa kwenye timu yake mpya kwani jitihada zake zinambeba na anaamini atafanya vizuri zaidi akiendelea kukazana.
"Tuna furaha kuona Diogo anafanya vizuri, vilevile nilifanya kazi na nyota huyo kwa muda wa misimu minne hakuwa msumbufu ni anafanya kazi yake kwa wakati na nina amini kwamba atazidi kuwa bora.
"Anafurahia mpira, yupo kwenye wakati wa furaha kwa sasa ndani ya Liverpool na anafanya maajabu mengi ndani ya uwanja ninaamini hata kocha wake Klopp (Jurgen) anafuraha ya kweli dhidi yake," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment