November 19, 2020


 SERGIO Ramos beki mahiri ndani ya Klabu ya Real Madrid inayoshiriki La Liga ambaye ni mpiga penalti wao pia namba moja amewekwa kwenye rada za mabosi wa Klabu ya PSG inayoshiriki Ligue 1.


PSG inaamini kuwa ikipata saini ya nyota huyo mwenye mwili jumba itazidi kuwa imara zaidi ndani ya uwanja na kupata matokeo chanya kwenye mashindano ambayo watashiriki.


Mabosi wa PSG wameweka mezani kititta cha pauni milioni 18 ili kumpata Ramos raia wa Hispania mwenye miaka 34 na ipo tayari kumpa mkataba wa miaka minne tofauti na mabosi wake wa sasa Madrid ambao wao dili lao wanalotaka kumpa ni la mwaka mmoja.


Mkataba wa Ramos unakamilika mwisho mwa msimu huu hivyo ikiwa hataongezewa mkataba mwingine itakuwa dili jepesi kwake kuibukia ndani ya PSG licha ya kwamba Kocha Mkuu wa Madrid, Zinedine Zidane anahitaji huduma ya beki huyo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic