November 5, 2020

 


IMEELEZWA kuwa nyota namba moja ndani ya Yanga kwa uzalishaji wa mabao kwa wageni Carlos Carlinhos hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Simba, Novemba 7, Uwanja wa Mkapa.


Raia huyo wa Angola ametengeneza jumla ya pasi mbili za mabao yaliyofungwa na Lamine Moro ambaye ni kinara wa mabao kwa mabeki ndani ya Bongo.


Aliumia akiwa mazoezini wakati timu yake ilipokuwa kambini kwa maandalizi ya mechi ya ligi dhidi ya Polisi Tanzania kwenye enka na mpaka sasa anaendelea kupambania afya yake irejee kwenye ubora.


Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Shecky Mgazija amesema kuwa hali ya nyota huyo imetengamaa ila itakuwa ngumu kwake kuanza kwenye kikosi kitakachomenyana na Simba.


"Carlinhos yupo vizuri na anaendelea salama lakini hataweza kuwa kwenye kikosi kitakachocheza na Simba kwa kuwa hajafanya mazoezi muda mrefu hivyo hayupo fiti," amesema.


Yanga ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 9 kibindoni ina pointi 23 inakutana na Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi zake ni 19 zote zimecheza mechi 9.


Chanzo:Championi

4 COMMENTS:

  1. Hata Kama angekuwepo kipigo kipo pale pale

    ReplyDelete
  2. Mechi za Dabi hazitabiliki. Kuwa makini na kauli yako itakutokea puani

    ReplyDelete
    Replies
    1. anaongea tu kama kaoka usingizini, Mkwasa huyu aliyemtoboa juz ndiye alimtoboa janual 4 akiwa na kikosi butu tena bila kocha mkuu kabla ya Luc Emael kuja.
      sasa leo anajisahaulisha.
      jambo la msingi Kaze aache woga

      Delete
  3. Kaze hawezi kuiogopa Simba kwa sababu yupo na kocha mdaidizi Juma Mwambusi aliyeweka historia akiwa pia kocha msaidizi na kuitungua Simba 2 kwa bila mara mbili enzi za Pluijm.Simba wajiandae Kisaikolojia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic