MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wale ambao wanawabeza kuhusu uwezo wao wakikutana ndani ya uwanja watawapapasa na kuwakung'uta.
Ruvu Shooting imecheza jumla ya mechi 10 na kukusanya pointi 16 ikiwa nafasi ya tano huku kinara akiwa ni Azam FC mwenye pointi 25.
Ikiwa imeshinda mechi nne kati ya hizo ilikuwa ni dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba, Uwanja wa Uhuru kwa kuifunga bao 1-0 na Coastal Union pia ilikutana na kibano Uwanja wa Uhuru kwa kufungwa mabao 3-1.
Bwire amesema:-"Ni utaratibu mzuri uliopo ndani ya Ruvu Shooting, unajua kuna mabadiliko makubwa hasa kwa upande wa mfumo pamoja na uongozi hivyo lazima kila kitu kiende kwa ustaarabu na umakini mkubwa.
"Tunamjali kila mmoja mpaka mpishi naye muda wote anakuwa na furaha kuanzia kwenye masuala ya malipo na ushirikiano ni mkubwa.
"Usisahau kwamba tuna mwalimu mzuri mwenye mipango makini ndani ya uwanja, hatuna hofu sisi ni mwendo wa kupapasa, kukung'uta na kutoa dozi kwa wapinzani ambao watakuwa wanatubeza tutakutana uwanjani," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment