November 8, 2020


 ANTONIO Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wachezaji wa Simba walicheza chini ya kiwango kwenye mchezo wa dabi jana Novemba 7 kwa kuwa walikutana na wachezaji wenye kiwango bora.


Yanga walikamilisha raundi ya 10 bila kufungwa ndani ya Ligi Kuu Bara waliweza kusepa na pointi moja mbele ya Simba ambayo imepoteza mechi mbili.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ilianza kufunga bao la kuongoza dakika ya 31 kupitia kwa Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalti baada ya Joash Onyango kumchezea faulo Tuisila Kisinda na mwamuzi wa kati Abdalah Mwinyimkuu kuamuru ipigwe penalti.


Simba ilipata bao la kuweka usawa dakika ya 86 kupitia kwa beki Onyango baada ya kumalizia mpira wa kona iliyopigwa na Luis Miquissone wengi hupenda kumuita Konde Boy.


Nugaz amesema:"Kweli Simba imecheza chini ya kiwango kwa kuwa imekutana na timu yenye wachezaji ambao wana kiwango kikubwa zaidi yao.


"Tuliwatamani sana Oktoba 18 tukawakosa ila kwa kuwa walikuja Novemba 7 tulikutana nao ila tumeweza kuona namna gani timu inacheza na mbinu ambazo Kaze yupo nazo." 

13 COMMENTS:

  1. Wamefurahi kuwa wamepata droo kwasababu hawajategemea

    ReplyDelete
  2. Hahaha Nugaz kweli kupiki basi la mwendo kasi ndio kiwwngo cha juu kweli mlicheza kiwango cha juu sana ndio refa akakupeni penati ya nje ya box. Endelezeni kuwa na refa mchezaji

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mfumo ulihitaji hivyo hebu kuwa muelewa kidogo

      Delete
  3. Yaani Simba wakicheza chini ya kiwango ndio wanakuwa sawa na Yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Miaka zaidi ya 3 Yanga inalalamikia Marefa na ninyi mikia mlikuwa mnawabeza na kusema wamezidi kulalamika. Sasa ninyi hili moja tu mnavunja rekodi ya kulalamika. Hakuna asiyejua udhaifu wa marefa wetu na wanafanya hayo ni kudhihirisha kuwa uwezo wao wa kutafsiri sheria ni mdogo. Msilalamike kuwa Yanga inabebwa wakati nayo inalalamika mara nyingi tu. Ninyi mmesema Yanga inabebwa kwa kuangalia mechi ya Jana tu. Mbona wakat Yanga inalalamika ninyi mnasema Yanga wanalalamika mambo ya uongo. Kuweni weledi basi kukemea udhaifu wa marefa ili tuinue kiwango cha soka Tanzania. Hiyo TFF ambavyo imejaa Simba tupu wanawezaje kuweka marefa wenye mikakati ya Kuipendelea Yanga wakati wao wooooootee mpaka wafagiaji ni Wanasimba?

      Delete
  4. Miaka zaidi ya 3 Yanga inalalamikia Marefa na ninyi mikia mlikuwa mnawabeza na kusema wamezidi kulalamika. Sasa ninyi hili moja tu mnavunja rekodi ya kulalamika. Hakuna asiyejua udhaifu wa marefa wetu na wanafanya hayo ni kudhihirisha kuwa uwezo wao wa kutafsiri sheria ni mdogo. Msilalamike kuwa Yanga inabebwa wakati nayo inalalamika mara nyingi tu. Ninyi mmesema Yanga inabebwa kwa kuangalia mechi ya Jana tu. Mbona wakat Yanga inalalamika ninyi mnasema Yanga wanalalamika mambo ya uongo. Kuweni weledi basi kukemea udhaifu wa marefa ili tuinue kiwango cha soka Tanzania. Hiyo TFF ambavyo imejaa Simba tupu wanawezaje kuweka marefa wenye mikakati ya Kuipendelea Yanga wakati wao wooooootee mpaka wafagiaji ni Wanasimba?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msimu uliopita penati aliyopewa Kagere baada ya kuguswa na Yondani nje ya box

      Delete
  5. hahahahaha nimecheka sana simba ikicheza chini ya kiwango ndo wanatoka dro na yanga daaah

    ReplyDelete
  6. Mikia inatakiwa mjue sikuzote team inayoshinda ndio inapaki bus, kipindi Cha pili Yanga ilikuambele kwa goli, kwahiyo walichofanya kuangalia uwezekano ya counter attacks sio kushambulia bila mipango, nakama washambuliaji wangekua vzr mngepigwa Sana.
    Pia mlikua mnasema hamuwezi kulalamikia maamuzi ya refa leo imekula kwenu mnalialia kama vile sio nyie mliopewa penati na Kagere akafunga, acheni lawama chezeni mpira, hapo kikosi kulikua hakina muunganiko kukiwa na muunganiko mtakufa mengi Sana...
    Daima mbele nyuma mwiko...

    ReplyDelete
  7. We zuzu unajua maana ya chini ya kiwango au unatapika tu upone maradhi yako.Yanga poleeni kama huyu ndo mwajiriwa wenu mnaetegemea kuisemea Yanga mh!! poleni hii nisawa mama aliyezaa mtoto wa kiume halafu akawa đŸ’‹, maana yake huyu alitoa uchafu tu tumboni

    ReplyDelete
  8. Ile Penalti ya Kagere, Kelvin Yondani alipaswa kupewa kadi nyekundu kama isingekuwa penalti kwa kuwa alicheza rafu akiwa yeye ni mtu wa mwisho, lakini penalti ya yanga faulo imefanyika nnje ya box na onyango hakuwa mtu wa mwisho, kulikuwepo kuna beki WAWA hivyo ilipaswa iwe free kick na sio penalti na Onyango alipaswa kupewa kadi ya njano BASI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kosa la penati ya Kagere halihalalishi kosa la penati ya Yanga Novemba 7. Hawa marefa wapumbavu sana! Kuna viashiria vya rushwa kwa hawa waganga njaa.

      Delete
  9. simba iko juu sana ikicheza chin ya iwango ndio inakua sawa ya yanga hongeren simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic