November 9, 2020

 


NYOTA saba wa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 wapo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo inakazi ya kucheza na Tunisia Novemba 13.


Mchezo huo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2021 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na nafasi ndani ya kundi j.


Tunisia ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi sita na imeshinda mechi zote mbili huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na pointi tatu.


Hawa hapa nyota wa Simba  waliopo ndani ya Stars ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein (Tshabalala), Jonas Mkude, Erasto Nyoni, John Bocco, Mzamiru Yassin na Said Ndemla.

 


7 COMMENTS:

  1. Ni saba au ni nane?

    ReplyDelete
  2. Itasaidia nini? Hata ungewachukua wote hatuna uwezo wa kuifunga Tunisia

    ReplyDelete
  3. nafasi ya ndemla angepewa dilunga mzee wa focus

    ReplyDelete
  4. Kaseke, shaibu, erasto na ndemla nadhani hawastaili kuitwa stars kwasasa....unamuachaje yule dogo Adamu adamu wa JKT?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapo Ndemla anastahili. Yupo vizuri sana. Adam Adam yumo kikosini.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic