November 16, 2020

 


SERGIO Ramos, nyota ndani ya Klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Hispania ameandika rekodi yake ya kuweza kucheza jumla ya mechi 117 na kuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi nyingi na timu ya taifa.


Kwenye mchezo wake wa Novemba 14 wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 aliweka rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 34.


Ramos ambaye ni beki na mpiga penalti namba moja ndani ya Real Madrid alikutana na kisiki cha mpingo kipa Yann Sommer ambaye aliokoa penalti mbili.


Hii ni rekodi yake pia ya kwanza kwa beki huyo kukosa penalti mbili kwenye mchezo mmoja ndani ya uwanja.


Amefunga jumla ya penalti 25 ikiwa ni ndani ya timu yake ya Taifa ya Hispania pamoja na Klabu ya Real Madrid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic