PASCAL Wawa, beki wa Simba amesema kuwa kabla ya mchezo wowote ule kuanza yeye hupenda kusali pamoja na kuskiliza muziki mzuri.
Raia huyo wa Ivory Coast mwili jumba kwenye mabao 22 yaliyofungwa na timu hiyo kwenye Ligi Kuu Bara amefunga bao moja.
Alifunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa anapenda muziki wa Tanzania ikiwa ni pamoja na nyimbo za King Kiba na Diamond.
"Napenda kuskiliza muziki mzuri kabla ya kuingia uwanjani na kila msanii ninakubali uwezo wake katika kazi anayofanya.
"Kusali kwanza pia ni muhimu kwangu napenda kufanya hivyo kila wakati," amesema Wawa.
Leo Simba itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.
mbona alimkanyaga NCHIMBI MAKUSUDI.
ReplyDelete