November 8, 2020


 SHOMARI Kapombe, beki wa kulia mzawa ndani ya Simba ambaye pia jina lake limetajwa kwenye majina ya wachezaji 27 kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije amesema kuwa wanaamini watatwaa ubingwa wa ligi.

Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambao waliutwaa msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kufikisha jumla ya pointi 88.


Baada ya jana Novemba 7 kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1inabaki nafasi ya tatu na pointi 20.




Kwenye mechi zote 10 ambazo Simba ilikuwa imecheza, Kapombe ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji na alitumia jumla ya dakika 824.

Msimu uliopita wakati Simba ikitupia jumla ya mabao 78 alihusika kwenye mabao sita ambapo alitengeneza jumla ya pasi sita za mwisho zilizoleta mabao.

Kapombe amesema:”Tuna kazi kubwa ya kufanya kwetu sisi wachezaji kutimiza majukumu yetu ndani ya uwanja, lengo letu ni kuona tunatwaa ubingwa na ili hilo liwezekane ni lazima tushinde mechi zetu.

“Kikubwa ninawaambia mashabiki waendelee kutupa sapoti katika kazi yetu kwani uwepo wao uwanjani unatuongezea nguvu,” amesema.

9 COMMENTS:

  1. Sina imani hivyo sijui lolote laweza tokea ila kwa hivi ninavyo ona mm kama mm na nimwanachama sina imani

    ReplyDelete
  2. Kapombe.ni.mchezaji anayejitolea kwa asilimia mia moja nina imani na kauli yake

    ReplyDelete
  3. Mwanachama namba ngapi? Isije ikawa Utopolo ni disguise.

    ReplyDelete
  4. Ni wewe huna imani ila wao kama wachezaji ndio wanaifanya hiyo kazi siyo wewe, kutokuwa na Imani kwako hakutabadilisha kitu

    ReplyDelete
  5. Miaka zaidi ya 3 Yanga inalalamikia Marefa na ninyi mikia mlikuwa mnawabeza na kusema wamezidi kulalamika. Sasa ninyi hili moja tu mnavunja rekodi ya kulalamika. Hakuna asiyejua udhaifu wa marefa wetu na wanafanya hayo ni kudhihirisha kuwa uwezo wao wa kutafsiri sheria ni mdogo. Msilalamike kuwa Yanga inabebwa wakati nayo inalalamika mara nyingi tu. Ninyi mmesema Yanga inabebwa kwa kuangalia mechi ya Jana tu. Mbona wakat Yanga inalalamika ninyi mnasema Yanga wanalalamika mambo ya uongo. Kuweni weledi basi kukemea udhaifu wa marefa ili tuinue kiwango cha soka Tanzania. Hiyo TFF ambavyo imejaa Simba tupu wanawezaje kuweka marefa wenye mikakati ya Kuipendelea Yanga wakati wao wooooootee mpaka wafagiaji ni Wanasimba?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msimu uliopita penati ya Kagere aliyopewa baada ya kuguswa na Yondani nje ya box

      Delete
  6. ni ngumu sna simba kutwaa ubingwa marefa wamepanga timu yao ya kubeba ubingwa

    ReplyDelete
  7. Ni mara ngapi mmeshindwa kuondoka na ushindi kwa sababu ya Marefa msimu huu? RUVU waliwafunga Uhuru, Prisons waliwatoboa Sumbawanga mbona hamkusema marefa wamezibeba timu hizo? Ninyi ni Walalamishi Fc

    ReplyDelete
  8. Safari hii mpenyo wa yule bosi wao kuhonga marefa kama misimu 3 iloyopita naona kama vile fungu limekata, saiz mo akiweka ugoko gsm anaweka shoka tutaelewana tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic