November 8, 2020

 


RICHARD Djod, kiungo wa Azam FC amesema kuwa kazi kubwa iliyobaki kwa wachezaji ni kutimiza majukumu ndani ya uwanja kwa kupata matokeo chanya.


Azam FC ni vinara ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 baada ya raundi 10 kukamilika, wameshinda mechi 8, kupoteza mchezo mmoja ilikuwa kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na kuambulia sare moja ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania.


Djod amesema kuwa kazi iliyopo kwa wachezaji wote kwa sasa ni kuendelea kupambana ndani ya uwanja ili kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zijazo.

"Msimu huu ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo kama ilivyo kwetu pia,jambo moja tunalotakiwa kufanya ni kuongeza juhudi na katika kusaka ushindi.


"Bado kuna mechi mbele yetu ambazo tunapaswa tucheze hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitakuwa sawa," amesema. 


Azam ikiwa imecheza mechi 10 ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ina pointi 25 inafuatiwa na Yanga nafasi ya pili na pointi zake ni 24 nafasi ya tatu ipo kwa Simba ikiwa na pointi 20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic