November 29, 2020

 


KIKOSI cha Simba, leo Novemba 29 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Plateau United kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa New Jos, nchini Nigeria wenye uwezo wa kuchukua jumla ya mashabiki 40,000 ulikuwa na visa vingi kwa wenyeji wakiwa na lengo na kuwatoa Simba mchezoni.


Bao la ushindi limepatikana dakika ya 53 kupitia kwa Clatous Chama kwa pasi ya Luis Miquissone ambaye alikuwa ni mwiba kwa Plateau United.


Miongoni mwa vikwazo ambavyo walikuwa wanaweka watu wa Nigeria ni pamoja na kuwabugudhi waandishi wa Habari wa Tanzania katika kufanya ripoti ya matukia.


Pia jana, Novemba 28 licha ya jitihada za uongozi wa Simba kuomba matangazo yarushwe mubashara kupitia Azam Tv jamaa waligoma na kuweka ngumu mpaka leo siku ya mchezo Azam Tv hawakupewa haki ya kutangaza mubashara zaidi ya kutangaza kupitia kwa radio.


Habari nyingine ni kwamba Simba walipigwa mkwara kwenye upande wa kutumia wapishi wao mwanzo na kuleta ubishi mkubwa na pia wakazusha na ishu ya Corona kwa nyota wa Simba ikiwa ni kwa Claotous Chama, Luis, John Bocco lengo moja tu kuwatoa Simba mchezoni.


Ushindi walioupata Simba ugenini si haba ikiwa watapmbana kupata ushindi Uwanja wa Mkapa Desemba 6 na ikishinda itapenya mpaka hatua ya mtoano.

12 COMMENTS:

  1. Mnyama kanguruma ugenini juu ya kila aina vitimbwi. Kutokana na ustaarabu wa Simba, wao watawafanyia watapokuja hapa

    ReplyDelete
  2. Hao washenzi wataondoka na mzigo mzito wa mabao watapokuja hapa na wala hawato fanyiwa figisu za aina yoyote licha ya kwamba watapata sapoti kubwa kutoka kwa mautopolo

    ReplyDelete
  3. Asante MUNGU kwa ushindi wa leo.

    ReplyDelete
  4. walaumu jezi walizovaa..wamevaa utadhani utopolo ya moja moja kama kipindi cha Zahera..Na mwaka huu mtaongoza hadi ngwe ya pili na bado kombe litapita kando

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kocha wenu wa Simba alishawahi kusema, mkicheza mechi 7, mtakuwa mnaongoza ligi,na wewe leo unasema yanga watao goza Hadi ungwe ya pili, huo ndo mwendo wa yanga mdogo mdogo mpaka kombeee

      Delete
  5. Safi na Hongera sana Simba SC, Mnyamaaa

    ReplyDelete
  6. Mungu nimwema narudia tena kuwapongeza Wachezaji, Kocha na Viongozi pamoja ya wasaidizi wote wa Simba Sc kwa mwanzo mzuri huko Ugenini.

    ReplyDelete
  7. Hii ndo Simbaaaaaa, wengine ni utopolooooooooooo

    ReplyDelete
  8. Inaleta raha Sana roho mbaya fc kimyaaa

    ReplyDelete
  9. Sandress. vizur Sana wachezaji wamepambana

    ReplyDelete
  10. Hakuna team pale....bora hata ruvu shooting au tz prison......hiyo team haina tofauti na mwadui msijisifu mikia....subirini mkutane na wazee wa hamsa hamsa.....5*3 Itawahusu MWAMEDI FC nyie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Endelea kusugua benchi kimataifa wacha wanaume tufanye yetu. *Baki nyumbani endelea kupika wakati mmeo anakutafutia nafac nawe mkewe mwakani ushiriki* mwanamke akiwezeshwa anaweza, tulia tutakuwezesha uwezo wakujibeba Hauna.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic