November 29, 2020


 BEKI wa kulia wa Klabu ya Yanga, Kibwana Shomari amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri hivyo ana matumaini ya kurejea uwanjani hivi karibuni.


Kibwana alipata majeraha ya bega wakati timu yake ilipokuwa ikisaka pointi tatu mbele ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex.


Mchezo huo uliochezwa Novemba 25, Yanga ilishinda bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Deus Kaseke. Kibwana hakuweza kumaliza dakika zote 90 alitolewa nje ili kupewa huduma ya kwanza.


Kibwana amesema:"Kwa sasa ninaendelea vizuri na nina amini kwamba nitareja uwanjani hivi karibuni kuendelea na kazi ya kusaka ushindi kwa ajili ya timu yangu.


"Matibabu ambayo nimepata yananifanya nizidi kuwa imara zaidi hivyo ni suala la kuendelea kuomba dua na kusubiri muda nitakaporudi uwanjani namna hali iakavyokuwa," amesema.


Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13 hawajapoteza mchezo wanafuatiwa na Azam FC ambayo imecheza mechi 12 ikiwa nafasi ya pili na pointi 25.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic