SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ataanza mchezo wa leo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye ulinzi kabla ya kushambulia.
Simba ipo ndani ya mji wa Jos ambapo saa 12:00 jioni itakuwa ndani ya Uwanja wa New Jos kusaka ushindi kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 4-9, Uwanja wa Mkapa.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji ameongeza kuwa malengo ya kuanza kujilinda ni kuwasoma wapinzani wake ili ajue mbinu za kuwavuruga zitakazomfanya ajue uimara wao pamoja na udhaifu ndani ya uwanja.
Uwanja wa Jos una uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000 ila hawatakuwepo ndani ya Uwanja kwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) limetoa muongozo wa kutaka mechi zichezwe bila ya mashabiki kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
"Tutaanza na kuimarisha ulinzi mwanzo ili tujue uimara na mapungufu ya wapinzani wetu, tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tutapambana kupata matokeo," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment