Anaandika Saleh Jembe
NAJARIBU kujiuliza maswali rundo lakini jibu ni moja tu kuwa mpira wa Afrika na hasa sisi chini ya Jangwa la Sahara umejaa upuuzi wa kipuuzi ambao unafanana sana.
Ishu yangu ni kuona Plateau United FC kuzuia mechi isionyeshwe LIVE kwa kuwa wana haki hiyo.
Swali la kwanza wanajua ni kipindi cha Covid 19
Pili wanajua mashabiki wao wangependa kuwaona wakipambana na SimbaTatu, runinga ni mapato na matangazo ya wachezaji.
Hakuna anayeshiriki kuendesha timu ya soka atasema hahitaji fedha.
Wakati mwingine unajiuliza hivi Plateau wanataka KUIDHULUMU Simba hadi wanakubali kupoteza kila kitu? WANATAKA KUWANYONGA SIMBA?
Nafikiri ni akili za hovyo na hata hazistahili kujadiliwa na inaonyesha kiasi gani soka la Nigeria ni UBABAISHAJI wa kiwango cha juu kupitiliza.
Wanigeria wanaoiogopa Simba kiasi hiki hadi kufanya mambo ya KIPUUZI kiasi hiki.
Hapo nakuvulia kofia. Basi hawatii akilini au ndio wamesahau kuwa na wao pia watakuwa huku baada ya siku cache na ubaya wanaowafanyia Simba na wao watafanyiwa kama huo
ReplyDeleteWamekosa weledi. Mpira unachezwa hadharani, hata usiporusha watu wataona na wengine watarekodi matukia yote yenye utata
ReplyDeleteNigeria siasa tu inawapa taabu
ReplyDeleteLabda walitaka wapewe rushwa, maana wamekubuhu ktk eneo hilo.
ReplyDeleteLeo ndio umesesa saleh wapumbavu hao washirina matapeli hao wasubiri kwa mkapa sasa waone cha moto
ReplyDeleteSisi wastaarabu na tutawapa starehe mpka wasikie aibu halafu tukiwafunga kila nao mpira upo live nigeria
ReplyDeleteVyema umelaumu tabia ya Waafrika kusini mwa Sahara. Juzi Tanzania walizima taa vyumba vya kubadilisha nguo timu pinzani. Kusini mwa Afrika upuuzi kama huu ni haba. Hamasisha kutolipiza kisasi. Wape huduma wachape uwanjani.
ReplyDelete