November 16, 2020


 KIKOSI cha Simba leo kimalazimisha sare ya bila kufungana na timu ya African Sports kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo langoni alikaa kipa namba tatu, Ally Salim na kuliweka lango lake salama ndani ya dakika 90.


Kwa upande wa safu ya ushambuliaji chini ya nyota Charlse Ilanfya imeshindwa kufurukuta kupata bao mbele ya Klabu ya African Sports.


Sven amefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha leo ambapo amewatumia vijana wengi chini ya miaka  20 ili kuwapa uzoefu.


Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na Hassan Mohamed,Omary Kazi, Isack Mohamed, Godfrey Mbomahenga, Seif Suleman na Hamis Manguka.


Wale wa kikosi cha kwanza ilikuwa ni pamoja na kiungo Clatous Chama,Francis Kahata, Ibrahim Ame, Kened Juma, Miraj Athuman, Rarry Bwalya na Beno Kakolanya. 

10 COMMENTS:

  1. Chama Tena si yupo na timu ya taifa? Kuwa serious kidogo

    ReplyDelete
  2. Hiyo timu ya taiga labda ya pemba

    ReplyDelete
  3. Kazi kulalamika tuu ungeanfalia mpira ndio ugejiuliza kuwa huyu ni chama au msukule wake

    ReplyDelete
  4. Walikuwepo chama,bwalya,ajibu,kahata,miraji,ilamfya ila matokeo ni bila bila inasemekana senzo kawahujumu tena wanampeleka tena police

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndo uwezo wao wacha tuone sinema zao za police huko. Mwandishi naye lialia wa simba huyu eti Mara under 20.... Duh! Juzi yanga hakuanza kuchambua nani alicheza

      Delete
  5. Wakati mwingine tutumie akili hata robo kijiko. Mambo ya senzo yanaingiaje hapa. Kama alihujumu watu wasiseme? Kwa hiyo kila simba akitoka sare au kupoteza hata hizi mechi za kupima timu nazo hadthi itakuwa senzo. Yanga mnakuwa kama watoto wadogo? Suala liko polisi subirini matokeo kama tunavyosubiri matokeo ya FIFA CAS na CAF kuhusu morrisson.

    ReplyDelete
  6. Lakini blog hii ndio iliyoandika kuwa chama kaitwa team ya taifa ya zambia baada ya kiungo tarajiwa wa team ya zambia kuwa na matatizo.Tena wakisisitiza simba kumuwekea ulinzi mkali,leo yuko dar,upuuzi gani huu.

    ReplyDelete
  7. Utopolo hamnazo, mechi za kirafiki mnajaji nazo. Tutumie nguvu nyingi wakati keshokutwa tu hapa tunamechi dhidi ya plateu klabu bingwa, tutumie nguvu tuongeze majeruhi. Ninyi wa mchangani mkitumia nguvu Ni sawa tu maana hamuendi popote pale.

    ReplyDelete
  8. Hahahhahaha senzo hafai Mpaka machi za kirafiki jamni tunamuomba atuachie timu yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic