November 17, 2020


 TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeendelea na maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa marudiano dhidi ya Tunisia unaotarajiwa kupigwa leo Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Stars inaburuza mkia kwenye msimamo wa Kundi J katika michuano ya kufuzu Afcon 2022, ikiwa imekusanya pointi tatu kwenye michezo mitatu, wakishinda dhidi ya Guinea ya Ikweta na wamepoteza dhidi ya Libya na Tunisia ambao ndiyo vinara wa kundi.


 Tunisia walikusanya pointi tatu juzi na kufikisha 9, baada ya kuichapa Stars bao 1-0 nchini Tunisia.

 

Sasa Stars inatakiwa ishinde leo Jumanne ili kupata matumaini ya kuwa miongoni mwa timu mbili zitakazofuzu kutoka katika kundi hilo. Hadi sasa timu tatu zimefungana pointi na kila timu ipo katika nafasi yake kutokana na kigezo cha matokeo yalikuwaje timu zilizofungana pointi zilipokutana ‘head to head’.


Haya ni baadhi ya mambo ambayo yakifanyika Stars inaweza kuibuka na ushindi mbele ya Watunisia leo.

 

KUTORUHUSU BAO LA MAPEMA

Kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 13, Stars waliruhusu bao la mapema lililofungwa dakika ya 17 baada ya mshambuliaji wa Tunisia Youssef Msakni kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari, bao ambalo lilidumu kwa dakika zote 90.


Stars haitakiwi kuruhusu bao la mapema kwenye mchezo wa leo ambalo linaweza kusababisha timu ikatoka mchezoni kutokana na presha ya kusawazisha kuongezeka


UMAKINI KATIKA KUZUIA MASHAMBULIZI YA KUSHTUKIZA (COUNTER ATTACKS)

Moja ya mbinu kubwa za timu zinazotoka Kaskazini mwa Afrika ni kutumia zaidi mashambulizi ya kushtukiza wanapo cheza ugenini na hii ni kutokana na kusheheni wachezaji wenye kasi na wanyumbulifu.

Hivyo safu ya ulinzi ya Stars lazima iwe makini na mashambulizi ya kushtukiza jambo ambalo linaweza kusababisha timu ikaruhusu mabao mepesi kwenye mchezo huo.

 

UMAKINI KATIKA KUPIGA PASI

Stars kwenye eneo la kiungo ilipoteza umakini katika mchezo wa kwanza, jambo lililosababisha pasi nyingi kukosa uelekeo, Jonas Mkude, Himid Mao na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ walikosa maelewano na kujikuta timu inaelemewa huku pasi zao nyingi walizopiga zikiishia kwa viungo wa Tunisia.


Benchi la ufundi likiongozwa na Etienne Ndayiragije akisaidiana na Selemani Matola na Juma Mgunda, wana kazi ya kurekebisha tatizo hili ili lisijirudie kwenye mchezo wa leo kwani kwa soka la kisasa eneo la kiungo ndiyo roho ya timu.

 

KUTORUHUSU FAULO ZA MARA KWA MARA KARIBU NA LANGO

Jambo ambalo Stars wanapaswa kuwa makini nalo kwenye mchezo wa leo ni kutocheza faulo karibu na lango lao, kutokana na Tunisia kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kupiga mipira ya adhabu ambayo inaweza kusababisha mabao ya mapema.


KUTUMIA FAIDA YA KUCHEZA NA MASHABIKI

Stars itakuwa na faida ya kucheza na mashabiki kwenye mchezo wa leo baada ya Caf kuruhusu mashabiki 30,000 kushuhudia mtanange huo tofauti na Tunisia ambao walicheza bila mashabiki.


Faida ya uwepo wa mashabiki kwenye mchezo wa leo kwa kiasi kikubwa itaongeza hamasa na morali kwa wachezaji hivyo hii itakuwa na faida kubwa kwa upande wa Tanzania.

 

KUTOCHEZA MCHEZO WA KUJILINDA MUDA WOTE

Moja ya mambo ambayo yaliinyima matokeo Stars kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Tunisia ni kutokana na vijana wa Ndayiragije kujikita zaidi kwenye kujilinda kuliko kushambulia kwani kwa dakika zote 90, Stars haikupiga shuti lolote lililolenga lango huku mashuti yasiyolenga lango yakiwa mawili.


Kwenye mchezo wa leo ni lazima mwalimu Etienne aingie na mbinu ya kushambulia na kujilinda ambapo anaweza kuanza na mastraika wawili kwenye eneo la ushambuliaji ili kuinyima utulivu safu ya ulinzi ya Tunisia


UMAKINI KWENYE SAFU YA ULINZI

Licha ya kuruhusu bao kwenye mchezo wa kwanza, Stars ilikuwa bora kwenye eneo la ulinzi chini ya mkongwe Erasto Nyoni ambaye alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwatuliza mabeki wenzake kama Bakari Mwamnyeto.


Uwepo wa beki mzoefu kama Nyoni utachangia kwa kiasi kikubwa makosa mengi kutofanyika kwenye eneo la ulinzi jambo ambalo litaiweka Stars sehemu salama kwenye mchezo huo


3 COMMENTS:

  1. Tatizo kubwa la taifa stars kubwa kuliko yote ni upangaji wa kikosi sahihi na substution ama uweledi wa haraka wa kumtoa mcjezaji asifanya vizuri uwanjani na kumuingiza mchezaji sahihi wa kwenda kusahihisha makosa.Sio siri ila Tomasi Ulimwengu,Khasani Dilunga,Muzamir,Ndemla hawa ni baadhi ya wachezaji ambao walishapata changamoto za mechi za kimataifa ni wazoefu inashangza kuona wakikaa benchi na kuwaamini wachezaji wasio na uzoefu. Kwenye kiungo nadhani mapema tu atafutwe mchezaji mwengine badala ya mkude kwani anaonekana hayuko fiti labda abalike.

    ReplyDelete
  2. Dah nilitamani kumwona ulimwengu uwanjani leo,baada ya kurudi mazembe amekuwa bora

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic