November 17, 2020



LIVERPOOL ina matumaini ya kumtumia nahodha wao Jordan Henderson pamoja na Andy Robertson kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City jumapili kwa kuwa wamekuwa wakilindwa ili wasipate majeraha.

Wachezaji wote wawili walikuwa na hofu ya kupata majeraha ndani ya timu zao za Taifa ambapo Henderson anayecheza timu ya England pamoja na Robertson wa Scotland wamewekwa kando ili kulindwa.

Henderson alitolewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England Jumatatu huku Robertson akiwa ana imani kwamba ataondolewa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Israel. 

Kocha Mkuu wa Scotland, Steve Clarke ameweka wazi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa nyota huyo kuwa nje ya mchezo ili kumuepushia presha ya kuhofia kupata majeraha ndani ya uwanja.

"Upo uwezekano wa Rob kutoanza kwenye mchezo wetu kwa kuwa inaonekana ni kujihatarisha zaidi juu yake, lakini bado tuna matumaini ya kumuona pia akiwa uwanjani kwani ni mchezaji wetu muhimu," amesema. 


Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England mambo yamekuwa magumu kwao kwa sasa kutokana na kuwa na wachezaji wengi ambao wanasumbuliwa na majeraha.


Beki wao kisiki Virgil van Dijk, Fabinho, Joe Gomez na Joel Matip ni miongoni mwao na inatajwa kuwa watakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu isipokuwa Fabinho anaweza kurejea uwanjani baada ya wiki mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic