MCHEZO wa Novemba 14 Uwanja wa Mkapa kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania na Tunisia huenda ukachezwa bila ya uwepo wa mashabiki baada ya Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kutoa taarifa kwamba mechi zote zitachezwa bila ya uwepo wa mashabiki.
Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari jana jioni Novemba 6 imeeleza kuwa makubaliano hayo yamefanywa kupitia mkutano wa viongozi kwa njia ya video ikiwa na malengo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mkutano huo ulifanyika Novemba 4 kwa viongozi wa Caf kujadili namna bora ya kuendesha masuala ya soka ndani ya bara la Afrika ikiwa ni pamoja na maandalizi ya Afcon ambayo inatarajiwa kuchezwa nchini Cameroon 2021.
Caf pia imewataka wanachama kuwa makini katika usimamizi wa masuala ya usalama wa wachezaji pamoja na wahudumu ndani ya uwanja ili kuongeza usalama.
Kupitia kwa Dr.Christian Emeruwa ambaye ni mkuu wa kitengo cha masuala ya usalama ndani ya Caf amesema kuwa lengo kubwa la mpango huo ni kuona kwamba mechi zote zinachezwa katika hali ya usalama na umakini.
0 COMMENTS:
Post a Comment