WILLIAN da Silva, winga wa kikosi cha Arsenal amesema kuwa ana matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.
Wiga huyo ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho ambapo aliibuka ndani ya Arsenal akitokea Klabu ya Chelsea ambayo nayo pia inashiriki Ligi Kuu England.
Raia huyo wa Brazil mwenye miaka 32 amesema kuwa ana furaha kuwa ndani ya timu hiyo ambayo ina malengo makubwa jambo ambalo anaamini kuwa litamfungulia malengo yake ya mafanikio kwa kuwa hata familia yake inafurahia jambo hilo.
Ndani ya Chelsea ambayo ipo chini ya Kocha Mkuu, Frank Lampard, alidumu kwa muda wa misimu saba na kwa sasa ameiacha ngome ya Stamford Bridge yupo zake ndani ya Emirates akiwa chini ya nahodha Auba ambaye ni raia wa Gabon.
Willian amesema:"Ni furaha kwangu licha ya kwamba nimetoka ndani ya Chelsea hakuna cha kuniumiza kwa sasa kwani maisha ya mpira lazima yaendelee na hapa nilipo nina furaha hasa ukizingatia kwamba nipo na kocha Arteta ambaye ana mbinu nyingi na ninaamini tunaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England tukiwa chini yake.
"Arsenal ina kocha mzuri na mwenye uwezo mkubwa ikitokea tukashindwa kutwaa taji msimu huu inaweza kuwa msimu ujao hakuna tatizo kila kitu kinawezekana," .
0 COMMENTS:
Post a Comment