November 16, 2020


 KESHO timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ina kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa kufuzu Afcon 2021 dhidi ya Tunisia.


Stars ikiwa kundi J ina kibarua cha kupindua meza kibabe kwa kuwa mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 nchini Sudan.


Tayari wameshaanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa huku Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije akiweka wazi kuwa watatumia faida ya uwanja wa nyumbani kusaka matokeo.


"Tutakuwa nyumbani na nina amini kwamba utakuwa ni mchezo wenye ushindani lakini tupo tayari kufanya vizuri hivyo mashabiki watupe sapoti," amesema.

 Kwenye kundi J ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi tatu, imeshinda mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja inakutana na vinara wa kundi hilo ambao wana pointi tisa kibindoni.


Ili kufufua matumaini ya kuweza kufuzu Afcon ni lazima ishinde kesho ili kuongeza mtaji wa pointi kibindoni.


Mchezo wa kesho mashabiki wataruhusiwa kuingia ila sio kwa kiwango kikubwa kwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetoa muongozo kwa kuruhusu asilimia 50 ya mashabiki kuingia kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

5 COMMENTS:

  1. Taifa Stars haijacheza na Timu ya nchini Sudan kama mwandishi anavyoeleza aya ya Pili.

    ReplyDelete
  2. Huyu mwandishi anapenda sana Sudan,tangu aanze kutoa taarifa ya kufungwa stars amekuwa akichomekea neno Sudan kama sio kwenye kichwa cha habari utakuta kwenye body ya habari,sijui hafanyi uhariri kabla ya kupost.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiukweli nimekuwa mfuatiliaji wa page au blog hii kwa muda mrefu na imenisaidia sana kujua habari za michezo ila kama mwandishi ataendelea kuleta habari zenye mashaka au zisizo na vyanzo vya kuaminika nitalazimika polepole kurudi niliko toka. Naendelea kumshauri ahariri habari zake kabla ya kuleta kwa umma.

      Delete
  3. Himid Mao nimchezaji mzuri ila apunguze back pass ambazo sio za lazima,Nado alikuwa anapoteza mipira sana na kutoa pass hazina macho,Kapombe alikuwa anapanda sana na kuchelewa kurudi kwa wakati,Farid ni jembe.

    ReplyDelete
  4. Hahaaaa wasinge mtoa mwamnyeto I
    La na swali kevin yondani yukuapi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic