November 16, 2020


 MTAMBO wa kutengeneza mabao ndani ya Yanga,  Carlos Carlinhos amerejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda akitibu jeraha la enka.


Nyota huyo raia wa Angola alipata maumivu hayo wakati timu yake ikijiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa Uwanja wa Uhuru na Yanga kushinda kwa bao 1-0.


Jana, Novemba 15 alianza benchi kwa mara ya kwanza chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze wakati Yanga ikishinda mabao 3-1 dhidi ya African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki na alipata muda wa kucheza pia.


Ndani ya Yanga ambayo imefunga mabao 12 baada ya kucheza mechi 10 za ligi amehusika kwenye jumla ya mabao matatu akifunga moja na kutoa pasi mbili za mabao yote yakifungwa na Lamine Moro kwa kona ambazo alipiga.


Ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikishinda bao 1-0 na mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri wakati Yanga ikishinda bao 1-0.


Yanga ipo nafasi ya pili na pointi zake 24 kibindoni na vinara ni Azam FC wenye pointi 25 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 20.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wachezaji wote wapo vizuri taratibu wanarejea kwenye ubora. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic