TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, usiku wa kuamkia leo Novemba 18 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kushiriki Afcon.
Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni muhimu kwa Stars kushinda kwa kuwa ule wa kwanza ugenini ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 nchini Tunisia ulikuwa mgumu kwa Stars kwa kuwa walikubali kufungwa kipindi cha kwanza.
Zikiwa zimetofautiana dakika nane kwa kuwa mchezo wa kwanza Stars ilifungwa bao la ushindi dakika ya 18 leo Uwanja wa Mkapa imefungwa dakika ya 10.
Bao la kuongoza kwa Tunisia lilipachikwa kimiani na Saif Eddine Khaoul na kuongeza mzigo kwa Stars.
Iliwalazimu Stars kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja huku safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na nahodha John Bocco ikiwa haijafanya jaribio la hatari ndani ya dakika 45.
Bao la kuweka usawa na kuipa pointi moja Stars lilifungwa na Fei Toto ambaye alianzia benchi na alichukua nafasi ya Himid Mao dakika ya 47 kwa shuti kali akimaliza pasi iliyotengwa na Bocco.
Pointi hiyo moja inaifanya Stars iwe nafasi ya nne ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi nne huku Tunisia ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 10.
Nafasi ya nne ipo mikononi mwa Libya yenye pointi tatu na ile ya pili ni mali ya Equatorial Guinea yenye pointi 6 kwenye kundi J.
Hapa Umeandika Nini Sasa......
ReplyDeletePointi hiyo moja inaifanya Stars iwe nafasi ya nne ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi nne huku Tunisia ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 10.
Nafasi ya nne ipo mikononi mwa Libya yenye pointi tatu na ile ya pili ni mali ya Equatorial Guinea yenye pointi 6 kwenye kundi J.
Mwandishi ahariri habari kabla hajaileta kwa jamii
DeleteKabisa, point hiyo moja inaifanya stars owe nafasi ya tatu na sio y nne
DeleteImeisha ila kama ningekuwa Ndairagije basi kwenye safu yangu ya ushaimbuliaj ningemchezesha Saimoni Msuva kama sentafowadi namba 9 na namba kumi angecheza Muzamiru yasini Boko angeanzia benchi.
ReplyDeleteKuna shida ya upangaji kikosi cha stars hivi Adam Adam na Ulimwengu nani bora?.Mzee wa back pass Himid Mao kwnn alianza na sio Feisal?,Idd Nado mimi simkubali,Hivi kum
ReplyDeleteKumwacha Adam kama mshambuliaji tegemeo kocha alilenga nn?Tunisia team kubwa unaweka mtu wa kujifunza mpira,tunakazi ya kushinda ugenini kwa hao equetorial guinea kwao la sivyo biashara imeisha.
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania
ReplyDelete