November 30, 2020


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa namna ambavyo wameanza kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya mabingwa baada ya kushinda jana, Novemba 29 bao 1-0 mbele ya Plateau United wana imani watafika hatua ya makundi.

Kikosi hicho kinachonolewa na Sven Vandenbroeck kesho kinatarajiwa kuwasili Bongo baada ya kumaliza dakika 90 za mwanzo wakiwa ugenini nchini Nigeria wana dakika 90 nyingine Uwanja wa Mkapa.


Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, ambapo Simba inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele ila ikifungwa itakuwa na kibarua kizito cha kupata ushindi ikiwa, itafungwa bao moja zitaongezwa dakika na mshindi asipopatikana ngoma itakwenda matuta kwa kuwa itakuwa ni 1-1.

  Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa ushindi ambao wameupata na namna mazingira yalivyokuwa magumu yanawapa nafasi ya kupata matokeo mazuri na kupenya hatua ya makundi.


"Tumeanza vizuri na ni matumaini yetu kwamba ni Mungu amejibu maombi yetu hivyo kwa namna ambavyo tumepata ushindi katika mazingira tuliyopitia inamaanisha kwamba tutafika mbali.


"Kikubwa ninawapongeza wachezaji wetu kwa namna ambavyo wamepambana wanapaswa waendelee hivyo ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea," amesema.

10 COMMENTS:

  1. Mungu aweupande wetu kila wakati wa mashindano haya muhimu katika bara la Africa.

    ReplyDelete
  2. Eti unaandika Simba inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele, je ikitoka sare ya mbili mbili, je Simba itasonga mbele???? u?Hadi useme sare ya aina yoyote ile.????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duuu hatari simba kashinda ugenini sare ya aina yoyote simba anazonga mbele

      Delete
    2. Hata km ni sare 10-10 cmba unafuzu

      Delete
    3. Hata Sare ya 20-20 Simba ataendelea , ukiongeza goli waliloshinda Ugenini itakuwa 21-20

      Delete
  3. Hata kama zitatoka sare ya kufungana 10 kwa 10 Mnyama atasonga mbele

    ReplyDelete
  4. Simba wamepewa vibonde hawana ubora wowote ,,, yanga ndo timu pekee inayoweza kumpga Simba uwanja wowote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic