November 30, 2020

 


KIKOSI cha timu ya Taifa ya Uganda chini ya miaka 20 leo Novemba 30 kimetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Cecafa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo wa leo ambao umechezwa Uwanja wa Black Rhino Academy kipindi cha kwanza kilikamilika Uganda wakiwa mbele kwa mabao 2-0.

Mabao ya Uganda yalifungwa na Kenneth Semakula dk ya 23 na Avian Bogere aliyefunga mabao mawili dk ya 26 na 64.

Lile la Kenya lilifungwa na Enock Wanyama dakika ya 81. Ushindi wa Uganda unawafanya wamsubiri mshindi wa mechi kati ya Tanzania ambao ni wenyeji v Sudani ya Kusini utakaochezwa saa tisa na nusu Uwanja wa Black Rhino Academy. 


Fainali itachezwa Desemba 2.

5 COMMENTS:

  1. Uganda alicheza fainali na nani? Utoaji gani huu wa habari jamani? Kwenye chombo cha habari?

    ReplyDelete
  2. We ndo ujaelewa soma tena vizuri mbona mwandishi ameeleweka

    ReplyDelete
  3. Hajaleweka Uganda walicheza na nani nusu final?

    ReplyDelete
  4. Hii ni changamoto, yaandi mwandishi anashindwa kuandika match ni Kati ya team gan mwanzoni, badala yake anaweka mwisho kabisa, kama vile ni siri kujuA au chemsha bongo.
    Hili ni tatizo kama tusipo badilika Mambo mengi yataenda kienyeji, mwisho wasiku kuondoa mvuto hata kwa viewers wa site yenu...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic