November 4, 2020


 KIKOSI cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru.



Bao la kwanza kwa Simba limefungwa na nahodha John Bocco kwa mkwaju wa penalti baada ya mwamuzi kutafsri kuwa Hassan Dilunga amechezewa faulo na David Luhende ndani ya 18.


Bao hilo limepachikwa dakika ya 42 kwa mkwaju ambao ulimpoteza mlinda mlango Benedict Tinocco.


Iliwachukua dakika mbili Simba kufunga bao la pili kupitia kwa  Said Ndemla dakika ya 45+3 kwa pasi ya Clatous Chama.


Kipindi cha pili kilikamilika kwa timu zote mbili kumaliza dakika 45 bila kupata bao na kuifanya Simba ishinde mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic