November 15, 2020


 KIKOSI cha Yanga leo Novemba 15 kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Huu ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Kocha Mkuu, Cedric Kaze baada ya kupokea mikoba ya Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi, Oktoba 3.


Mabao ya ushindi kwa Yanga yamefungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 3, Yacouba Sogne dakika ya 7, Michael Sarpong dakika ya 28 kwa mkwaju wa penalti.


Bao la kufutia machozi kwa African Lyon lilifungwa na Mwalami Abdalah kwa mpira wa adhabu dakika ya 30 nje kidogo ya 18 na kuachia shuti lililomshinda mlinda mlango Ramadhan Kabwili.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic