November 7, 2020


LEO Novemba 7 Uwanja wa Mkapa ni Dar, Dabi kati ya Yanga v Simba saa 11:00 ikiwa ni ya kwanza kwa msimu wa 2020/21 kwenye Ligi Kuu Bara.


Zote zimecheza jumla ya mechi tisa ndani ya ligi na Yanga imeshinda mechi saba na kulazimisha sare mbili.Ipo nafasi ya pili na ina pointi 23.

Hizi hapa mechi za Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara:-

Yanga 1-1 Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.


Yanga 1-0 Mbeya City, Uwanja wa Mkapa.


Kagera Sugar 0-1 Yanga, Uwanja wa Kaitaba.


Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Uwanja wa Jamhuri, Moro.


Yanga 3-0 Coastal Union, Uwanja wa Mkapa.


Yanga 1-0 Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru.


KMC 1-2 Yanga, Uwanja wa Kirumba.


Biashara United 0-1 Yanga, Uwanja wa Karume.


Gwambina 0-0 Yanga, Uwanja wa Gwambina Complex.


Jumla Yanga imefunga mabao 11 na kufungwa mabao manne kinara wao wa pasi za mwisho ni Farid Mussa, Tuisila Kisinda na Carlos Carlinhos wenye pasi mbilimbili.


Kinara wa mabao ni Michael Sarpong, Tunombe Mukoko na Lamine Moro wenye mabao mawilimawili.

Simba imeshinda mechi sita kichapo mbili na sare moja ipo nafasi ya tatu na ina pointi 19. 

Mwendo wa Simba upo namna hii:-


Ihefu 1-2 Simba, Uwanja wa Sokoine


Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri, Moro.

Simba 4-0 Biashara United, Uwanja wa Mkapa.


Simba 3-0 Gwambina, Uwanja wa Mkapa.

JKT Tanzania 0-4 Simba, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.



Tanzania Prisons 1-0 Simba, Uwanja wa Nelson Mandela.


Simba 0-1 Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.


Simba 5-0 Mwadui FC, Uwanja wa Uhuru.


Simba 2-0 Kagera Sugar, Uwanja wa Uhuru.


Jumla Simba imefunga mabao 21 imefungwa mabao manne. Kinara wa utupiaji ni Meddie Kagere mwenye mabao manne anafuatiwa na Chris Mugalu mwenye mabao matatu.


Kinara wa pasi za mwisho ni Clatous Chama mwenye pasi tano na Luis Miquissone mwenye pasi tano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic