KIUNGO mzawa Feisal Salum, ameweka bayana kuwa wamekubaliana kupambana msimu wa 2020/21 kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 24, imefunga jumla ya mabao 12, kinara ni Azam FC mwenye pointi 25 na watani zao wa jadi Simba wamejenga ngome nafasi ya tatu na pointi 20, zote zimecheza mechi 10.
Kwa misimu mitatu mfululizo, Yanga imewashuhudia watani zake wa jadi Simba wakitwaa taji la ligi kuanzia msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2019/20.
Ndani ya Yanga, Fei Toto ambaye amecheza jumla ya mechi tisa na kuyeyusha dakika 779 uwanjani, ni miongoni mwa viungo bora kwa msimu wa 2020/21.
Kiungo huyo amesema: “Tunajua kwamba hatujachukua ubingwa miaka mitatu mfululizo, kwa sasa kazi imeanza, ninaamini kwamba tutafikia malengo ya kutwaa ubingwa na kurejesha furaha kwa mashabiki.”
Vita ya ubingwa inazidi kupamba moto kwa timu ambazo zipo ndani ya tatu bora ambapo kila timu kwa sasa inahitaji kutwaa ubingwa.
Mabingwa watetezi ni Simba nao wameweka bayana kuwa wanahitaji kutwaa taji hilo kwa mara nyingine tena.
Kuutaka ni kitu kingine na kuupata ni kitu kingine,kila mwaka wanautaka ila kuupata ndio imekuwa shida.
ReplyDelete