MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Simba, Charlse Ilanfya amesema kuwa ikiwa Kocha Mkuu wa timu, Sven Vandenbroeck atampa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza atafunga mabao mengi.
Ilanfya ameibukia ndani ya Simba akitokea Klabu ya KMC ambapo akiwa huko msimu wa 2019/20 aliweza kutupia mabao sita na kutoa jumla ya pasi tatu za mabao.
Maisha yake ndani ya Simba yamekutana na ushkaji na benchi kutokana na ushindani wa namba hasa kwa nafasi ambayo anacheza sambamba na nahodha John Bocco mwenye mabao manne sawa na Meddie Kagere.
Simba ikiwa imecheza mechi 10 za ligi ameanza kikosi cha kwanza mchezo mmoja na hakumaliza dakika 90 ilikuwa Uwanja wa Nelson Mandela wakati Simba ikionja joto ya kuyeyusha pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0.
Nyota huyo amesema:"Ikiwa kocha atanipa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza mara kwa mara ninaamini kwamba nitafunga mabao mengi kwa timu yangu.
"Kila mchezaji ni bora nami ninapambana kuwa bora na nikipata nafasi nitaonyesha uwezo wangu wa kufunga kwani hiyo ni kazi yangu."
Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 10 na namba moja ni Azam FC mwenye pointi 25 na ile ya pili ipo mikononi mwa Yanga wenye pointi 24.
Ajikaze na kuwa mbunifu zaidi na mpambanaji ana kipaji cha ajabu ila inaonekana akili yake hajaiekeza kukitambua kipaji chake ili kimtofautishe na wengine.Mpira ni kujiamini kwanza ukiachilia mbali kipaji na uwezo na ndio maana akina mbape na umri mdogo kabisa lakini ni panga pangua kila siku first eleven kwenye timu ya taifa na Klabu yake.
ReplyDeleteAmuige ndemla
ReplyDeleteAnakipaji sana ila anatakiwa kuwa mvummilivu na mwenye kujituma sana na ahakikishe anatumia vizuri nafasi anazopata mithili ya Mugalu.
ReplyDeleteCharles Ilafya anatakiwa afanye mazoezi ya binafsi pamoja na yale ya Kocha ili awezekuwa vizuri zaidi, tunahitaji akipewa nafasi afanye vizuri kama alivyoanza mwanzoni na awe anajitoa zaidi kwenye michezo yake sisi jamii tutampigania acheze. Mfano mzuri Mugalu tunaendelea kumuombea awe fiti acheze na kutupa matokeo.
ReplyDelete