December 2, 2020


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa utakosa huduma ya nyota wao Prince Dube ambaye alipata majeraha kwenye mkono Novemba 25,2020 Uwanja wa Azam Complex.

Raia huyo wa Zimbabwe ambaye ni mashine kwenye kucheka na nyavu ndani ya Azam FC, alipata majeraha hayo dakika ya 15 baada ya kugongana na beki chipukizi ndani ya Yanga, Bakari Mwamnyeto katika harakati za kuwania mpira wa juu.

Alishindwa kuendelea kwenye mchezo huo na alishuhudia timu yake ikiyeyeyusha pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 wakati akipewa huduma ya kwanza na jopo la madaktari wa Azam FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa taarifa kutoka nchini Afrika Kusini pamoja na ile ya awali waliyoipata kutoka kwa jopo la madaktri wa Muhimbili imeweka wazi kuwa nyota huyo atakuwa nje kwa muda wa wiki tano.


"Dube(Prince) baada ya kuumia alianza kupewa huduma ya kwanza na matibabu kwenye Hospitali ya Muhimbili ambapo huko aliweza kupata huduma na ripoti ilionyesha kwamba atakuwa nje kwa muda wa wiki nne mpaka tano.

"Hivyo kwa sasa tayari yupo nchini Afrika Kusini akiendelea kupewa matibabu, imani yetu ni kwamba atarejea kwenye uimara wake na kurudi kuendelea na majukumu yake.

"Mashabiki wasiwe na mashaka anapewa huduma nzuri na bado tunawasiliana naye ili kujua maendeleo yake yapoje," amesema.

Ndani ya Ligi Kuu Bara Dube ni miongoni mwa nyota watatu wenye mabao mengi ambapo kinara ni John Bocco wa Simba akiwa na mabao saba huku Dube, Ibrahim Meschack wa Gwambina na Adam Adam wa JKT Tanzania wametupia mabao sitasita kila mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic