December 2, 2020

 


IMEELEZWA kuwa Emmanuel Okwi anaweza kurejea tena ndani ya Klabu ya Simba ili kuendeleza huduma yake kikosini hapo kutokana na safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kusumbuliwa na majeraha.


John Bocco mwenye mabao saba, Meddie Kagere mwenye mabao manne na Chris Mugalu mwenye mabao matatu hawa ni chaguo la kwanza la Sven Vandenbroeck lakini wamekuwa wakikosekana kwenye baadhi ya michezo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.


Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United uliochezwa Uwanja wa New Jos nchini Nigeria, Bocco alianza na Kagere hakuweza kucheza kutokana na kukosa mechi fitnes.


Alishuhudia timu yake ikishinda bao 1-0 ugenini kupitia kwa Clatous Chama akiwa benchi.

Habari zimeeleza kuwa kutokana na mipango ya Simba kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika imeweka mpango wa kumrejesha Okwi ambaye ana maelewano mazuri na Clatous Chama, Meddie Kagere, John Bocco na Mohamed Hussein kwa kuwa alishacheza nao msimu wa 2018/19.


"Okwi bado yupo kwenye hesabu za Simba na wakati ukifika anaweza kurejea kikosini hivyo ni jambo la kusubiri na kuona kwani hata kwenye usajili wa dirisha kubwa alikuwa kwenye hesabu ila mambo yalikwama." ilieleza taarifa hiyo.


Msimu uliopita, Okwi aliweka ujumbe wa pongezi kwa Simba baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na kumuambia Chama kuwa anaamini wataonana hivi karibuni.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameweka wazi kwamba kwenye suala la usajili wataangalia ripoti ya mwalimu inasema nini kisha watashusha majembe ya kazi.

8 COMMENTS:

  1. Tafuteni wachezaji vijana, Okwi hawezi kuwa bado na uwezo kama wa awali

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa waache kusajili kwa mihemko watafute wachezaji vijana watakaokaa pamoja kwa muda mrefu. Hii ni SIMBA siyo Juventus jengeni kikosi chenye damu changa na sio kutujazia wahenga tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😄😄😄😄 Hawa Hawa mababu wanawatoa nishai.
      Huyo Saido.ni.kijana.kinaumri gani?

      Delete
  3. Mikia fc hamna akili kabisa, yan mmekosa striker mwingine mpaka Okwi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si useme tu moyo umeshtuka paaaaa! baada ya kusikia OKWINYO anarudi tena

      Delete
  4. Chukueni kijana Nchimbi

    ReplyDelete
  5. SIMBA siyo timu ya raggby Nchimbi Wa nini sasa,

    ReplyDelete
  6. SIMBA siyo timu ya raggby Nchimbi Wa nini sasa,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic