UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kwamba unahitaji taji la Kombe la Shirikisho ili kurejesha heshima kwenye viunga vya Azam Complex.
Kwa sasa taji hilo lipo mikononi mwa Simba ambayo jana ilikuwa
na kibarua mbele ya Majimaji ya Songea, Uwanja wa Mkapa kweye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Simba ilishinda mabao 5-0 kwenye mchezo huo na kuiondoa Majimaji kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho.
Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imetinga
hatua ya nne ya mashindano hayo baada ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Magereza ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mkoa wa Dar kwenye mchezo wa hatua ya tatu.
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya
Azam FC, Abdulkarim Amin, amesema kuwa wanahitaji kufanya vizuri kwenye kila
mashindano watakayoshiriki ili kuweza kutwaa mataji.
“Kwenye kila mashindano ambayo tunashiriki malengo yetu ni kushinda, hivyo kazi bado inaendelea na kwenye Kombe la Shirikisho pia tunahitaji kufanya vizuri ili kuweza kutwaa taji kwani hilo linawezekana,” amesema Amin.
Ubingwa wa VPL mmeushindwa? Azam kombe lenu LA Mapinduzi haya mengine yana wenyewe
ReplyDeleteUbingwa wa VPL mmeushindwa? Azam kombe lenu LA Mapinduzi haya mengine yana wenyewe
ReplyDelete