December 28, 2020

 


BONIFACE Pawasa, beki wa zamani wa Simba, amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibazonkiza ni habari nyingine kwenye soka la Bongo kutokana na uwezo alionao.

 

Ntibazonkiza ni ingizo jipya ndani ya Yanga akiwa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara, amefunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao.

 

Mchezo wake wa kwanza ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji ambapo alifunga na kutoa pasi moja na mchezo wa pili ulikuwa ni dhidi ya Ihefu, hapo alitoa pasi mbili za mabao.

 

Pawasa amesema kuwa amemtazama nyota huyo kwenye mechi alizocheza na kugundua kwamba ni miongoni mwa usajili mzuri uliofanywa na Yanga kwa miaka ya hivi karibuni.

 

"Ntibazonkiza ni mchezaji mzuri, kwa aina yake ya uchezaji anaonekana kuwa imara kwa sababu hana uchoyo wa pasi na anajua kutengeneza nafasi, hivyo mabeki lazima wawe makini wanapokutana naye kwani muda wowote anaweza kubadili matokeo.

 

"Kuwa na mchezaji ambaye ana uwezo wa kubadili matokeo muda wowote ni hazina kwa timu. Ninaamini kwamba ikiwa hatapata majeraha kwa wakati huu kutakuwa na mengi ambayo atayafanya ndani ya uwanja,” amesema Pawasa.


Chanzo:Spoti Xtra

1 COMMENTS:

  1. Safi sana mkongwe....mimi huwa napenda falsafa ya kuongea ukweli hasa tunapojadili kuhusu soka,lakini utakuta kuna watu ambao mimi huwa nawaita mashabiki maandazi(awe wa simba au yanga) wao kazi yao kuponda tu hata kama mtu anauwezo lakini kwasababu si mchezaji wa upande wake yeye anaponda tu....wafundishe ushabiki wa soka unavyopaswa kuwa.
    Mimi ni shabiki mkubwa wa yanga lakini kuna wachezaji ambao wanavipaji viziru na ninawakubali siku zote kwa kuwataja wachache tu ni Chama,Luice,Ajibu,Dilunga na wengineo.


    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic