December 26, 2020

 


KIKOSI cha Azam FC leo Desemba 26 kimetinga hatua ya nne kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya tatu dhidi ya Magereza FC.

Azam FC imeshinda kwa jumla ya mabao 2-0 na kuwafanya wakamilishe dakika 90 wakiwa washindi huku mlinda mlango wao Wilbol Maseke akilinda lango lake bila kufungwa.

Mashabiki wa Klabu ya Azam FC walishuhudia mabao hayo yakipachikwa na Obrey Chirwa dakika ya 24 na Never Tigere dakika ya 65.


Azam iliugawa mchezo kwa vipindi viwili ambapo kipindi cha kwanza Chirwa  alipachika bao hilo kwa kichwa akitumia kona ya Never Tigere.


Kipindi cha pili Azam ilipata bao kupitia kwa Tigere ambaye amekuwa nyota wa mchezo wa leo akihusika kwenye mabao yote mawili, akifunga bao la pili na kutoa pasi moja ya bao.


Taji la Kombe la Shirikisho kwa sasa lipo mikononi mwa Klabu ya Simba ambao kesho watakuwa na kazi ya kuanza kutetea kikombe hicho mbele ya Majimaji ya Songea, Uwanja wa Mkapa.

6 COMMENTS:

  1. Uandishi wa ajabu sana. Husemi azam kacheza na timu gani sasa hupni kama habari inahang tuu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yan hawa jamaa kwa ubabaishaji..Ni kweli, hawajasema Azam wamecheza na timu gani, so kwa mtu ambaye hakufuatilia kabla ya mchezo hii habari haitamsaidia kabisa... Huu ni mwendelezo wa ukanjanja wa blogu hii

      Delete
    2. Mbona ameandika dhidi ya magereza fc, mwanzo kabisa

      Delete
  2. Kuna watu wamezoea kulaumu tu wamevulugwa na timu zao

    ReplyDelete
  3. Hvi nyie mnalalamika mbona kama vile akili zenu ni mavi tu, mwandishi kasema kabisa kwa Azam wametinga hatua ya Nne dhidi ya magereza fc! Nyie mtakuwa mashabiki wa nguruwe fc

    ReplyDelete
  4. Wewe umekuta amebadili taarifa (ameedit) baada ya kukumbushwa ndio unaona yuko sawa, mwanzoni haikuwa vile. Acha matusi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic