December 26, 2020

 


UWANJA wa King Power, mchezo wa Ligi Kuu England wababe wawili wametoshana nguvu ndani ya dakika 90 kwa kufungana mabao 2-2.


Kipindi cha kwanza wachezaji wote walikwenda vyumba vya kubadilishia nguo wamekiwa wamefungana bao 1-1 ambapo Marcus Rashford alianza kutupia dakika ya 23 likasawazishwa na Harvey Barnes dakika ya 31.


Kipindi cha pili kila timu ilikuwa ikipambana kusaka ushindi ambapo United kama kawaida yao walianza kupata bao la kuongoza.

 Bruno Fernandes dakika ya 79 alipachika bao la pili kwa United ambalo likasawazishwa na Jamie Vardy dakika ya 85.


Dakika 90 zimekamilika kwa miamba hii miwili kugawana pointi na kila timu kutupia mabao mawilimawili.


Matokeo haya yanaifanya United ikiwa imecheza mechi 14 kuwa nafasi ya tatu na pointi 27 huku Leicester City imecheza mechi 15 ikiwa nafasi ya pili na pointi 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic