December 2, 2020


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa makosa ambayo yalitokea kwenye mchezo wao dhidi ya Biashara United watayafanyia kazi ili kupata matokeo kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC. 

Azam FC ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 13, imekusanya pointi 26 na kufunga mabao 19.


Desemba 7 ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Gwambina FC mchezo utakaochezwa Uwanja wa Gwambina Complex.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa licha ya kwamba watakuwa ugenini kwa namna ambavyo wamekuwa na mashabiki Mwanza ni sawa na kuwa nyumbani na mazingira ya hapo wanayamudu vema.

"Tupo nyumbani kwa wakati huu na mashabiki wapo wengi ambao wamejitokeza kutupa sapoti, mechi sita zilizopita tumepata pointi tano tofauti na zile saba za awali ambapo tulipata pointi 21.

"Mechi muhimu kwetu tunataka kutumia kurudisha morali, kwa sasa tupo Mwanza tutapambana kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Gwambina.

"Mchezo wetu uliopita tumegundua mengi ambayo tutayafanyia kazi kwani tulikuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda ila haikuwa hivyo zaidi wapinzani wetu walikuwa nao kwenye ushindani mkubwa," amesema.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic