KIUNGO mkabaji (defensive midfielder) wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda Taddeo Lwanga amesaini dili la miaka miwili kuitumia Klabu ya Simba na leo Desemba 2 ametambulishwa rasmi.
Nyota huyo amewahi kuzichezea timu za Express FC, SCV Kampala, Vipers FC na Tanta FC hivyo uzoefu wake na uwezo wake ndani ya uwanja ni sababu ya kupewa dili ndani ya Simba.
Nyota huyo alikuwa kwenye rada za mabosi hao kwa muda mrefu baada ya kiungo wao Gerson Fraga raia wa Brazil kupata majeraha ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Fraga aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United na nafasi yake ilichukuliwa na Said Ndemla ambaye ni mzawa.
Usajili wa Lwanga unatokana na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kutoa nafasi za wawakilishi wa mashindano ya kimataifa kusajili wachezaji 10 ili kuongeza nguvu katika mashindano hayo.
Usajili mzuri, ukuta ukijengwa fresh Hamna kutetereka hiyo.
ReplyDeleteTusunasubiri kuona matendo uwanjani...
ReplyDeleteHalafu mukashindane na mazembe viungo wa kujipiga ganji tieni pesa hakuna mchezaji humo
ReplyDeleteHii post ya mwisho lazima ni ya Utopolo. Mavi yanagonga chupi.
ReplyDeleteHamna hiyo ya nguruwe fc ila hapendi kudanganywa kama tunavoambiwa chama milioni 700 wakati hatuna mchezaji wa hata milioni 200 tuache uwongo
ReplyDeleteNyani f.c mnachekesha
DeleteNguruwe fc hapo hamna mchezaji, mbona ametemwa na TANTA FC? kwahiyo hapo kiufupi tu mmepigwa
ReplyDeleteHapo sema kweli uongozi umekosea bora ungeanza kuboresha safu ya ulinzi sasa huyu mchezaji ana nn jipya zaidi ya kufunga lile gori la mbali zidi ya gormahia hapo kweli tumepigwa na kwa nn Tanta alicheza mechi 11 tu akatemwa?
ReplyDelete👆👆👆 akili zenu bdo makinda hatuwashangai, mkipevuka akili mtaacha utopolo
ReplyDeleteUbora wa timu yake ya taifa unambeba, Uganda wako juu kisoka kuliko sisi. Mnaweza kusema alitemwa kumbe walishindana masilahi. Kuwa kiungo wa timu ya taifa ya Uganda ni dhahiri kiwango chake kizuri pia.
ReplyDeleteJamaa yupo vizuri tena Sana.Mbabe wa soka analijua vizuri na mwili unamruhusu.
ReplyDelete