December 21, 2020

 


IMEELEZWA kuwa beki wa Klabu ya Mtibwa Sugar,  Hassan Kessy amewekwa kwenye rada za mabosi wa kikosi hicho ili kumrejesha kundini.

Kessy alikuwa kwenye hesabu za kujiunga na Yanga msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake na Klabu ya Nkana FC ila mambo yalibuma kutokana na ishu ya dau kuwa kubwa.

Kwa sasa yupo zake Mtibwa Sugar akiendelea kusaka ugali wa kila siku kupitia kazi yake hiyo anayoipenda kwa wakati huu.

Habari zimeeleza kuwa Kocha Mkuu Cedric Kaze anamtazama beki huyo ili aweze kumuunganisha ndani ya kikosi hicho kwenye usajili wa dirisha dogo ambalo limefunguliwa Desemba 16.


"Kaze amepewa jukumu la kufanya usajili kwa wachezaji ambao anahitaji na kwa namna kikosi kilivyo nadhani hakutakuwa na usajili wa kutisha zaidi ya kuboresha kidogo tu.

"Miongoni mwa nyota ambao anawafuatilia ni pamoja na Kessy,(Hassan) hivyo akikubali uwezo wake anaweza kurudishwa kundini," ilieleza taarifa hiyo.

Kaze kuhusu usajili amesema:"Kwa sasa ngoja nimalize hizi mechi ambazo zipo mbele yangu nikitulia nitazungumza na uongozi nini kinahitajika,".

3 COMMENTS:

  1. Wakati mwingine huwa mnatulazimisha wasomaji tutoe maneno ya shombo kwa habari zenu za kipuuzi

    ReplyDelete
  2. Hahahaha mwandishi umejitungia tu wala hizo taarifa hazipo, jaribu kuwa unafanya utafiti wa kina kabla ya kukupuka kuandika, huu ni upuuzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic