December 21, 2020




EDWARD Manyama, beki wa kushoto wa Klabu ya Namungo inaelezwa kuwa amewekwa Kwenye rada za Simba na Yanga.

Yanga walianza kumvutia kasi mzawa huyo ambaye aliwahi kucheza pia kwenye kikosi hicho ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambacho kinawania ubingwa.


Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze kinaongoza Ligi Kuu Bara na kibindoni kina pointi 40 na kimecheza jumla ya mechi 16.

 Beki huyo wa kushoto ni mtaalamu pia wa kupiga mipira iliyokufa ambapo walipokutana na Azam FC, Uwanja wa Azam Complex alimtungua kipa namba mbili Benedict Haule kwa faulo aliyoipiga akiwa nje kidogo ya 18.


Habari zinaeleza kuwa Simba nao wapo kwenye hesabu za kuwania saini ya beki huyo ili akamuongezee changamoto Hussein Mohamed ambaye kwa sasa anapambana na Gadiel Michael.


Kuhusu usajili ndani ya Yanga, Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo amesema kuwa jukumu lote lipo mikononi mwa kocha ambaye anajua anahitaji aina gani ya wachezaji.

7 COMMENTS:

  1. Bora aende yanga kwa huyu kocha wetu atakaa benchi tu hat mechi ya kirafiki hatacheza

    ReplyDelete
  2. Hakuna na nafasi wakati ule.wakati mwngne unapokosa nafasi katk timu bora kusaka maisha Mahal kwngn huo ndo mpira

    ReplyDelete
  3. Uongozi unasema jukumu hilo ni la kocha,kwenye habari ya kesi kocha anasema ngoja amalize mechi za raundi ya kwanza ndio atakaa na uongozi,kisha wachezaji wapo kwenye rada.ya mayai changanya na matembelele juu unamwagia maziwa mgando,ndio waandishi wa leo.

    ReplyDelete
  4. Sim a atacheza wapi au ndo akaozee bench

    ReplyDelete
  5. Waandishi wetu hao kesho watakuja na kichwa cha habari kinasema SUALA LA MANYAMA KUTAKIWA SIMBA NA YAMGA LIKO NAMNA HII, ukisoma hiyo habari utakuta timu zimekanusha kumtaka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic