December 5, 2020


 KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, alikuwa katika benchi akishuhudia timu yake ikipata kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya PSG, katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Pamoja na kipigo hicho, kuna jambo limeibuka kuwa katika mchezo huo kiungo wa United, Bruno Fernandes inadaiwa alikuja juu na kufoka akitaka kocha afanye mabadiliko wakati mchezo ukiendelea.

 

Picha zinamuonyesha Bruno akifoka huku akionyesha ishara ya kunyanyua mkono, japo bado uhakika wa nini alichokuwa akifoka lakini inadaiwa alikuwa akitaka atolewe mshambuliaji Marcus Rashford ambaye alikuwa ameumia.

 

Kipigo hicho kilichotokea kwenye Uwanja wa Old Trafford, kimeiacha United katika wakati mgumu katika mbio za kufuzu hatua ya mtoano kwa kuwa timu tatu kati ya nne zinalingana pointi.

 

Mashabiki wengi wa United mtandaoni wameonekana wakimshushia lawama Ole kuwa alikuwa mgumu kufanya maamuzi ya mabadiliko  kuanzia kwa Fred ambaye hakuwa na mchezo mzuri mwisho akapata kadi nyekundu.

1 COMMENTS:

  1. Ole Gunnar timu imemzidi uwezo utd wangefanya maamuzi magumu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic