December 5, 2020


 VIRGIL Van Dijk ameonyesha picha zake kwa mara ya kwanza akifanya mazoezi baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Everon ambapo aligongana na kipa katika harakati za kutaka kufunga.

Beki huyo kisiki mwenye umri wa miaka 29 inaelezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja msimu mzima akitibu mejaraha ambayo ameyapata kwenye sare ya kufungana mabao 2-2, Uwanja wa Goodson Park kwenye Merseyside Derby Oktoba 17.

Tangu Oktoba 17 amekuwa nje ya uwanja akipata matibabu ili kurejea kwenye ubora wake baada ya kufanyiwa upasuaji jambo ambalo linaleta matumaini kwa mashabiki wa Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England licha ya hofu kwamba atakosa mechi zote za msimu huu wa 2020/21.

Amekosekana kwenye mechi kadhaa za Liverpool ikiwa ni pamoja na ile ya sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Brighton pamoja na ule wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ajax ambapo Liverpool ilishinda bao 1-0.

Dijk ametuma ujumbe kwamba anafanya juhudi zaidi ili kuweza kuwa bora na ambapo alifanya mazoezi hayo hivi karibuni akiwa kwenye sehemu mpya ya kufanya mazoezi kwa timu yake ya Liverpool ndani ya Kirkby. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic