December 5, 2020

 


LUKAS Kikoti nahodha wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo utakuwa ni wa marudio baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Namungo FC kushinda mabao 3-0.

Wakati wakiwa nyumbani waliweza kushinda kwa kupitia Stephen Sey ambaye alifunga mabao mawili na bao la tatu lilifungwa na Shiza Kichuya.

Wapinzani wao kutoka Sudani ya Kusini wameamua kutumia Uwanja wa Azam Complex kutokana na masuala ya kisualama hivyo Namungo mchezo wa pili watakuwa wageni licha ya kwamba wapo nyumbani na mashabiki wao.

Kikoti amesema kuwa maandalizi yapo vizuri wanaamini watapambana kupata matokeo chanya kwenye mchez huo. 


"Tupo tayari na kila mchezaji anatambua kwamba utakuwa ni mchezo wa ushindani hilo halitupi tabu tutajituma kupata ushindi kwenye mchezo wa marudio.


"Kikubwa ni kwamba kila mmoja anatambua jukumu lake hivyo tutaingia ndani ya uwanja kwa nidhamu na tutajituma zaidi," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic