December 21, 2020


MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Simba,(CEO) Barbara Gonzalez amesema kuwa suala la Shiza Kichuya limesitishwa kwa kuwa Fifa walijua kwamba wanawasiliana na mtu ambaye hayupo ndani ya Simba.

Hivi karibuni habari zilieleza kwamba nyota huyo wa zamani wa Simba amefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita kutokana na kukiuka masuala ya usajili wake na Simba kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Kichuya ambaye alirejea ndani ya Simba akitokea Klabu ya Pharco ya Misri ambao inaelezwa kuwa waliishtaki Simba kwa kumsajili mchezaji akiwa bado na mkataba jambo ambalo liliwafanya Fifa kumpiga pini nyota huyo huku Simba ikitakiwa kulipa faini ndani ya siku 45.


Barbara kuhusu suala hilo amesema:-“Suala la Kichuya, Fifa wanatutendea haki. Tuliwaandikia na kuwaambia hatushirikishwa lolote na kulikuwa na mtu anawasiliana na Fifa nje ya klabu.


"Sasa tunasubiri barua ya Fifa kwa maana ya mashitaka na wametuandikia barua kuwa tuendelee na shughuli zetu, Shiza ni mchezaji huru na Simba inaweza kuendelea kusajili.


“Fifa nao waligundua waliyekuwa wanawasiliana naye si mtendaji wala kiongozi wa Simba na Kichuya unaona anaendelea hadi hapo tutakapopokea barua kutokea Fifa,” .


Kwa sasa Kichuya anaendelea na maisha yake ndani ya Klabu ya Namungo FC ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

8 COMMENTS:

  1. Yana mwisho na tutamjua t nan kaleta huu utata ila niisifu safu nzima y uongozi wa clab y Simba sc kwa utulivu mkubwa waliotuonyesha ktk kulifuatilia hili jambo wanatuonyesha kweli tim inaenda kweny mabadiliko pamoja na kuwepo waandishi wajuaji sana tena kuna walioonyesha wanalijua hili kuliko at hao FIFA wenyewe mtendaji mkuu kaonyesha kitu tafaut san tangu afike ndan y Simba.kila la kheri j.5 uko Zimbambwe.

    ReplyDelete
  2. Bila ya uoga nasubutu kusema kuwa Ismail Adeni Rage kawa msaliti wa Simba hivi sasa na ni miongoni mwa maadui wanaoiombea club ya Simba majanga. Katika suala hili la kichuya Rage amekimbilia na kukurupuka kuanza kuulaum uongozi wa Simba kana kwamba alikuwa na uhakika wa Jambo alilokuwa akilaumu. Kuna taarifa kuwa Rage ndie aliekuwa anamtia kiburi kigwangala na kauli zake za kijinga kuhusu uekezaji ndani ya simba mpaka kuonekana wa hovyo. Maulidi wa Kitenge na Wachambuzi wake pale wasafi media Mara nyingi wamekuwa wakiwapotosha wasikilizaji wao kwa
    kuwalisha habari zisisokuwa na ukweli, yaani kama Simba itaamua kuwafikisha mbele ya vyomno vya Sheria kudai fidia kwa kuchafuliwa kwenye suala la kichuya basi wasafi media wanayo kesi ya kujibu. Watu waache kukurupuka na kuanza kulaum Bila kusikiliza pande ya pili kwenye Jambo ambalo linahusisha pande mbili.Vita zidi ya kuihujumu Simba is real na wanasimba wanatakiwa kuamka na kusikiliza maelekezo kutoka kwa uongozi wao wa club badala ya kuhemkwa na habari za mitaani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kweli,kwani wapi FIFA imekanusha kuandika barua? Viko wapi vielelezo vinavyothibitisha hayo anayoyasema CEO wa Simba?

      Delete
  3. Bila shaka huyu ni senzo na timu yake kutoka ule upande aliokimbilia. Kitenge ndio ajenti wao hao wanaharakati dhidi ya klabu ya simba.

    ReplyDelete
  4. Kuna mashetani na vibwengo, hawaitakii mema SSC....!!

    ReplyDelete
  5. Watachonga sana, Simba mwendo mdundo fitina za zitawala wenyewe

    ReplyDelete
  6. Mi nadhani huyo Dada anawadanganya Kuna siku mtasikia mapya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic