December 21, 2020


KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kuwa msimu wa 2020/21 una ushindani mkubwa jambo ambalo linawafanya wapambane kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

Ruvu Shooting imekuwa kwenye mwendo wa kuvutia kwa msimu wa 2020/21 ikiwa ipo ndani ya tano bora kwenye msimamo.

Inashikilia rekodi ya kuwa timu ya pili kupeleka maumivu kwa mabingwa watetezi Simba ilipokutana Uwanja wa Uhuru kwa ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mkwasa amesema kuwa kila siku wanajipanga ili kufanya vizuri kwenye mechi zao zote ndani ya uwanja.

"Tunatambua kwamba ushindani ndani ya ligi ni mkubwa nasi tunapambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

"Mashabiki waendelee kutupatia sapoti kwa kuwa kila mchezo ambao tunaingia kucheza ndani ya uwanja kwetu ni fainali," .

Mchezo wake uliopita alikiongoza kikosi hicho Uwanja wa Azam Complex kupindua meza mbele ya Azam FC na kufanya matokeo kuwa sare ya kufungana mabao 2-2. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic