KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa anahitaji kuona timu inapata pointi tatu ndani ya uwanja suala la kushinda mabao mengi sio jambo kubwa.
Yanga imeshinda mechi zake mbili mfululizo a kusepa na pointi tatu huku ikishinda bao mojamoja ambapo ilikuwa dhidi ya Azam FC na JKT Tanzania.
Kaze amesema:"Mchezo wa leo utakuwa mgumu hasa ukizingatia kwamba tunakutana na timu ambayo ipo imara na ina mwalimu mzoefu ambaye yupo vizuri kiukweli.
"Nasi pia tumejiandaa kwa uzuri ninadhani kwamba mechi itakuwa na mvutano mkubwa lakini tumejiandaa kupata pointi tatu muhimu.
"Kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu kwanza ambazo tunazitafuta hivyo ninaomba mashabiki watupatie sapoti," amesema muda mfupi kabla ya mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
Mtupiaji namba moja ndani ya Yanga ni Michael Sarpong mwenye mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.
0 COMMENTS:
Post a Comment