December 6, 2020


 KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Yanga na wanawaheshimu wapinzani wao hivyo hawana mashaka katika kusaka pointi tatu.

 Mkwasa amesema hayo muda mfupi kabla ya timu yake kuingia Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu dhidi ya Yanga.


Mkwasa amesema:"Tunaingia ndani ya uwanja tukijua kwamba tunakutana na vinara wa ligi, hilo lipo wazi lakini nasi pia tumejipanga kuona kwamba tunapata matokeo mazuri.

"Burudani ni kitu ambacho tumekuwa tukikifanya lakini ni katika kusaka matokeo mazuri ndani ya uwanja, tunahitaji pointi tatu nasi tupo tayari.


"Kikubwa mashabiki watupe sapoti na kuona namna gani tunaweza kuwa bora na kuzidi kuendelea kutoa burudani ndani ya uwanja," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic