December 2, 2020

 


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Ajax kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ni moja ya ushindi mkubwa ndani ya Europe kutokana na hali inayopitia kikosi chake.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Anfield usiku wa kuamkia leo, Klopp alishuhudia bao pekee la ushindi likifungwa na Curtis Jones dakika ya 58.


Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kuwa vinara wa kundi D baada ya kufikisha pointi 12, mechi tano ambazo walicheza wameshinda nne na kupoteza mchezo mmoja.


Wapinzani wao Ajax wapo nafasi ya tatu na pointi 7 kwenye mechi 5 walizocheza wameshinda mbili na kupoteza mbili huku wakiwa na sare moja na anayeburuza mkia ni Midtjlland mwenye pointi moja na nafasi ya pili ipo kwa Atalanta yenye pointi 8.


"Kiukweli kabisa tangu nipo ndani ya Liverpool ninaamini kwamba miongoni mwa mchezo mkubwa niliokutana nao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ni huu, bila mashabiki ndani.


"Hatujawahi kufanya namna hii, ilikuwa ngumu na muhimu kwetu, wachezaji waliweka ulinzi jiwe sijui niseme nini?

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic