December 2, 2020


 MABOSI wa Yanga inaelezwa wametenga dau la milioni 30 kuipata saini ya mshambuliaji namba moja wa JKT Tanzania, Adam Adam mwenye mabao sita na pasi moja ya bao kati ya 12 yaliyofungwa na timu yake.


Nyota huyo alikuwa wa kwanza kufunga hattrick ya kwanza msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara. Aliwatungua Mwadui FC kwenye ushindi wa mabao 6-1 Uwanja wa Mwadui Complex.

Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa ya nyota huyo kuingia rada za Yanga ni kutatua ubutu wa safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Michael Sarpong mwenye mabao matatu.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ameweka bayana kwamba ni lazima wafanye mchujo wa washambuliaji wake ambao wanashindwa kufanya vizuri ili kumpata mbadala wake.

"Kiuhalisia matokeo ambayo yanapatikana ndani ya uwanja ni mazuri kwa kuwa tunapata pointi ila kwa upande wa washambuliaji bado haijawa vizuri hivyo ni lazima mchujo ufanyike.

"Nafasi kwenye mechi zetu tunapata nyingi hasa kipindi cha kwanza, kwa mfano kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania tulipata nafasi tatu ndani ya dakika 45 ila tumefunga moja kuna namna inabidi ifanyike," amesema.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela kuhusu suala la kumsajili Adam wa JKT Tanzania amesema kwamba bado wanasubiri kuona ripoti ya mwalimu.

"Kuhusu Adam kumsajili ndani ya Yanga kwa sasa mambo bado, tunasubiri ripoti ya mwalimu ili kujua yeye anasemaje," .

11 COMMENTS:

  1. Dah mara hii Sarpong anatafutiwa mbadala? Kulikoni? Au Hersi wa GSM aliuziwa mbuzi kwenye gunia? Lakini Kocha Kaze alikiri amehusika kusajili wachezaji wa chama letu Yanga, mbona mashabiki na wanachama hatuelewi tena?

    ReplyDelete
  2. Yanga Kama mnaweza ili kuua kabisa tatizo msajilini, Makambo...Okwi...meddie Kagere na kichuya....hapo kwishaaaa

    ReplyDelete
  3. Hawa wabajuandikia tu kwa sababu hakuna kiongozi wa Yanga aliyetoa orodha ya majina ya wachezaji wanaoachwa. Pia Yanga ina nafasi kadhaa za kuongeza wachezaji wa ndani na nje kwa hiyo wanaweza kusajili bila kuwaondoa wachezaji waliopo. Waandish wengi wanaandika uchochezi ili habari zao zisomwe sana kwani wasipoandikia kuhusu vilabu vikubwa au wachezaji wakubwa habar zao hazitapata wasomaji wengi.

    ReplyDelete
  4. Ndio mana mnaambukia magarasa. Mchezaji gani wa nje menye kiwango cha mataifa mtampata kwa hizo mlizomtengea za milioni 30. Inaonesha na Chama ni kama hizo ndizo mlizomtengea. Hahaha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dismas Ten alituaminisha kwa video clip kuwa Clatous Chama tayari ameshasajiliwa na Yanga. Nugaz naye akasema "time will tell" Chama ni mali ya Yanga. Viongozi wetu watatuua kwa presha kutokana na uwongo wao. Sasa limeibuka la Sarpong na Yacouba kuwa kocha anaona hawampi kile anachokihitai kwenye kikosi kutokana na uwezo wao wa kufunga magoli wakiwa mstraika waliosajiliwa kwa kazi hoyo

      Delete
  5. Utopolo mzimu wamanji inawatafuna, rudini mkamwombe radhi mkopesheni team miaka10 maana toka asepe mpaka leo mmekuwa.mdebwedo.

    ReplyDelete
  6. Mil.30 labda mumrudishe Yikpe🙉🙉🙉🙉

    ReplyDelete
  7. Kichekesho Sarpong mmemdajili kwa milioni 180 hawapi matokeo, Adam Adam kwa vile Mbongo mnamtengea milioni 30. Acheni kudharau carrie za watu, mpeni m 180 ili awafanyie kazi ya thamani. Na wachezaji wa kibongo amkeni msikubali kununuliwa kwa hela ya madafu wakati mnapiga kazi kuliko magarasa hayo!

    ReplyDelete
  8. Hizi habari za kuungaunga, where is the source of information?

    ReplyDelete
  9. Ila kweli dharau m30 HV c bora ukae tu huko jkt kaka kukiko uende huko ukatukanwe tukanwe bure na kuishia benchi on a hats waziri Jr alivyoisha?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulitaka wacheze wote waliosajiliwa? Mbona ninyi Sheva mmemuua kipaji chake?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic