December 17, 2020


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amefichua kuwa hafikirii kufanya usajili wa kukurupuka katika kipindi cha dirisha dogo wala kuingia kwenye presha ya mashabiki kwani amepanga kutafuta wachezaji wenye uwezo mkubwa.

 Tayari dirisha dogo la usajili limefunguliwa jana Desemba 16 na Shirikisho la Soka Tanzania na unatarajiwa kufungwa Januari 15,2021.


 Yanga tayari imepanga kuwatoa baadhi ya wachezaji kwa mkopo ili waweze kusajili wachezaji wapya ambao wanaamini watakuwa na msaada.

 

 Kaze amesema kuwa anajua wanakwenda kwenye kipindi cha usajili lakini hatokubali kufanya usajili wa presha kwani amepanga kuchukua wachezaji watakaokuwa na uwezo wa kumsaidia katika kikosi chake.


“Najua kwamba tunaelekea katika usajili wa dirisha dogo ambalo nitalitumia kufanya maboresho katika maeneo ambayo naamini kwa sasa hayapo sawa, ligi ngumu kutokana na ushindani uliopo lakini haiwezi kuzuia kuwa na timu imara.

 

“Siwezi kusajili kwa sababu presha ya kile ambacho watu wanakiona, nataka kuchukua wachezaji ambao naamini wana sifa za kuisaidia timu kwa sababu katika kipindi hiki inakuwa ngumu kupata mchezaji bora kwa kuwa wengi bado wanafungwa na mikataba katika timu zao na ikishindikana, nitamaliza na hawa ambao tupo nao,” amesema Kaze.


Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 15, nafasi ya pili ni Simba ina pointi 32 ikiwa imecheza mechi 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic